Zelensky kukutana na Waziri Mkuu wa Ireland
13 Julai 2024Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ireland Simons Harris hii leo katika uwanja wa ndege wa Shannon ulioko magharibi mwa Ireland.
Mazungumzo hayo yatakuwa ni ya mara ya kwanza baina ya mataifa hayo mawili kufanyika huko Ireland na yatajikita katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.
Soma zaidi.Korea Kaskazini yakosoa tamko la mkutano wa kilele wa NATO, linaloishutumu kwa kuisaidia Urusi
Katika mazungumzo hayo, Harris anatarajiwa kutoa salamu zake za pole kwa Waukraine kutokana na vita hususan shambulizi la hivi karibuni la kulipuliwa kwa hospitali kubwa kabisa ya watoto nchini Ukraine mapema wiki hii na kumhakikishia msaada zaidi rais Zelensky.
Pia atamuelezea Zelensky kuwa Ireland inaiunga mkono kikamilifu Ukraine katika juhudi zake kutaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.