1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky kukutana na viongozi wa Ujerumani na Ufaransa

Sylvia Mwehozi
16 Februari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuwasili mjini Berlin na Paris hii leo na kukutana na viongozi wa mataifa hayo mawili na atatia saini mikataba ya usalama.

Scholz na Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani mwakajanaPicha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuwasili mjini Berlin na Paris hii leo na kukutana na viongozi wa mataifa hayo mawili. Akiwa mjini Berlin, Zelensky atakutana na kutia saini mikataba ya ushiriikiano wa kiusalama na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani. Kisha baadae ataelekea mjini Paris kwa ajili ya kutia saini mikataba kama hiyo na Rais Emmanuel Macron.

soma:Biden and Scholz kujadiliana juu ya msaada mpya kwa Ukraine

Zelenskyy pia anatarajiwa kushiriki katika mkutano wa usalama wa Munich unaoanza mwishoni mwa juma hili, ambao utahudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali wapatao 40 pamoja na wataalam wengi wa kijeshi.

Ziara ya Zelensky katika mataifa hayo makubwa ndani ya Umoja wa Ulaya, inafanyika wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukiingia mwaka wa tatu huku vikosi vyake vikikabiliwa na hali ngumu upande wa mashariki.

     

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW