1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky kuwahutubia maseneta wa Marekani kwa msaada zaidi

5 Desemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa hii leo kutoa hotuba kwa njia ya video mbele ya maseneta wa Marekani kwa kuhimiza msaada zaidi.

Volodymyr Volodymyr Zelensky wakati wa mkutano wake wa pamoja na Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel
Rais wa Ukraine Volodymyr Volodymyr Zelensky wakati wa mkutano wake wa pamoja na Rais wa Baraza la Ulaya, Charles MichelPicha: AFP/Getty Images

Hotuba hiyo ataitoa katika mkutano wa kulihimiza Baraza la Congress kuidhinisha mpango wa karibu dola bilioni 106 kwa ajili ya vita vya Ukraine, Israel na mahitaji mengine ya kiusalama.Ikulu ya White House imesema inakaribia kukosa pesa za kusaidia Ukraine ikiwa hatua ya haraka haitachukuliwa na kwamba hilo litainufaisha Urusi katika uvamizi wake nchini humo.Katika barua kwa Spika wa Bunge hapo jana, mkurugenzi wa bajeti waRais Joe Biden, Shalanda Young amesema muda unayoyoma kuisaidia Ukraine. Hayo yakijiri, Urusi imeendeleza mashambulizi yake sehemu mbalimbali nchini Ukraine hasa katika mji wa Avdiivka.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW