1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky kuwasilisha "mpango wa ushindi" kwa EU na NATO

Sylvia Mwehozi
17 Oktoba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy anatarajiwa kuwasilisha "mpango wake wa ushindi" kwa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami NATO mjini Brussels hii leo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskiyPicha: AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy anatarajiwa kuwasilisha "mpango wake wa ushindi" kwa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami NATO mjini Brussels hii leo. Zelensky pia atawasilisha ombi la uanachama wa NATO na ongezeko la msaada wa kijeshi katika kampeni yake dhidi ya uvamizi wa Urusi. Mpango wa Zelenskiy unajumuisha maombi ambayo washirika wa Ukraine hadi sasa wamekataa kuyakubali, kama vile wito wa kualikwa kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO na ruhusa ya kutumia silaha za Magharibi kushambulia ndani ya Urusi.

Kiongozi huyo aliwasilisha mpango huo mbele ya bunge la Ukraine siku ya Jumatano mnamo wakati vikosi vya Moscow vikizidi kusonga mbele upande wa mashariki. Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte alisema wanachama 32 wa jumuiya hiyo wataupitia mpango huo kwa kina ili kuuelewa vyema. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW