1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky: Lazima Ukraine iwe chonjo na Belarus

11 Januari 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Ukraine lazima iwe chonjo katika mpaka wake na mshirika wa Urusi, Belarus, hata kama inaona kauli nzito zikitolewa kutoka kwa jirani yake huyo.

Ukraine Präsident Selenskyj
Picha: Ukrainian Presidential Press Service/REUTERS

Zelensky ameyasema hayo leo baada ya kulitembelea eneo la Lviv ambako amezungumzia ulinzi wa mpaka, hali ya usalama kaskazini magharibi mwa Ukraine na hali ya operesheni katika mpaka na Jamhuri ya Belarus na hatua za kukabiliana na mashambulizi katika maeneo hayo.

Afisi ya Zelensky imesema rais huyo pia ameshiriki shughuli ya kuwakumbuka wanajeshi wa Ukraine waliouwawa katika mapigano kufuatia uvamizi wa Urusi mwezi Februari mwaka uliopita.

Mapiganao makali yameripotiwa leo huko Soledar.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW