1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Zelensky: Marekani ikipunguza ufadhili, tutashindwa vita

20 Novemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nchi yake itashindwa vita vyake dhidi ya Urusi ikiwa Marekani itapunguza ufadhili wa kijeshi kwa Kyiv.

Zelensky (kushoto) akiwa na rais mteule wa Marekani Donald Trump
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (kushoto) akiwa na rais mteule wa Marekani Donald TrumpPicha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Hata hivyo Zelensky amesema wataendelea kupambana kwa kuwa wana uzalishaji wao wa silaha ingawa hautoshi.

Soma pia: Zelenskiy: Mwaka 2025 kuamua atakayeshinda vita Ukraine

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amekuwa akionyesha kupinga hatua ya utawala wa Biden kuipatia Ukraine mabilioni ya dola tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi. Haya yanajiri wakati Marekani imeidhinisha kuipatia Ukraine mabomu ya kutegwa ardhini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW