1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky: Mkoa wa Kharkiv umerejea katika hali ya utulivu

16 Mei 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hali ya utulivu imeanza kurejea katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv, baada ya kushambuliwa vikali na vikosi vya Urusi.

Volodymyr Zelensky
Rais Volodymyr Zelensky wa UkrainePicha: Gints Ivuskans/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hali ya utulivuimeanza kurejea katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv, baada ya kushambuliwa vikali na vikosi vya Urusi.

Rais Zelensky ambaye amelazimika kuahirisha safari zake zote za nje kutokana na vita hivyo kushika kasi, na ambapo wiki hii alitarajiwa kufanya ziara katika mataifa ya Ureno na Uhispania amesisitiza kuwa ikiwa Ukraine itawezeshwa kikamilifu, ni wazi kwamba watamshinda adui.

Katika siku za karibuni, Urusi imekuwa ikizidisha mashambulizi yake katika maeneo ya kusini na kaskazini-mashariki mwa Ukraine. Hayo yanajiri wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili China leo Alhamisi kukutana na mwenzake Xi Jinping akitafuta uungwaji mkono zaidi kutoka Beijing katika juhudi zake za vita nchini Ukraine lakini pia kufufua uchumi wake unaokabiliwa na vikwazo vya nchi za Magharibi.