1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky na Pistorius watembelea wanajeshi wa Ukraine

12 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius wamewatembelea askari wa Ukraine ambao wanapewa mafunzo ya kutumia mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot nchini Ujerumani.

Volodymyr Zelenskyj anatembelea eneo la mafunzo ya kijeshi la Ujerumani
Volodymyr Zelenskyj anatembelea eneo la mafunzo ya kijeshi la UjerumaniPicha: Jens Büttner/dpa/picture alliance

Wawili hao mchana Jumanne walitembelea eneo la mafunzo ya kijeshi huko kaskazini mwa Ujerumani. Eneo halisi halikufichuliwa kwa ajili ya sababu za kiusalama. Zelensky amesisitiza kuwa angalau mifumo saba zaidi ya Patriot inahitajika kulinda miji ya Ukraine dhidi ya mashambulizi ya anga ya Urusi. Zelensky aliwasili Berlin siku ya Jumanne, ambapo alishiriki mkutano wa kimataifa wa ujenzi mpya wa nchi yake na kisha akatoa hotuba kwa bunge la Ujerumani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW