1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky aahidi kuendelea kufanya mageuzi Ukraine

Angela Mdungu
4 Novemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa Ukraine imedhamiria kuendelea kufanya mageuzi yakiwemo ya kupambana na ubadhirifu.

Rais wa Halmashauri Kuu ya EU Ursula von der Leyen na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Halmashauri Kuu ya EU Ursula von der Leyen na Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Zelensky ameyasema hayo katika mkutano na wanahabari akiwa na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen mjini Kyiv.  Von der Leyen yuko ziarani nchini humo siku chache kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Umoja wa Ulaya kuhusu hatua zilizofikiwa na Ukraine katika juhudi zake za kutaka kujiunga na Umoja huo.

Soma zaidi: Von der Leyen: Umoja wa Ulaya utasimama na Ukraine hadi mwisho

Wakati huo huo, Marekani na maafisa wa Ulaya wamezungumza na serikali ya Ukraine kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa mazungumzo ya amani yenye uwezekano wa kumaliza vita. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Marekani la NBC lililowanukuu maafisa wa juu wa Marekani  ambao majina yao hayakuwekwa wazi.  Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine umeshasababisha maelfu ya vifo na majeruhi tangu vilipoanza miezi 21 iliyopita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW