1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Kiev: Urusi haina tena nguvu ya kufanya mashambulizi makubwa

18 Septemba 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Urusi haina tena nguvu ya kufanya mashambulizi mengine makubwa kwa kuwa imepoteza askari wengi baada ya zaidi ya miaka mitatu na nusu ya vita.

Paris 2025 | Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa mjini Paris Ufaransa baada ya kukutana na mwenzake Emmanuel Macron katika Ikulu ya Elysée: 03.09.2025Picha: Julien Mattia/Le Pictorium/MAXPPP/picture alliance

Zelensky ameendelea kuwa Urusi iliendesha operesheni kubwa nne mwaka huu nchini Ukraine katika majimbo ya Sumy, Novopavlivka, Pokrovsk na Zaporizhzhya, akisema kuwa baadhi tayari zimeshindwa huku akivisifu vikosi vyake.

Urusi na Ukraine  zimekuwa zikitoa mara chache takwimu juu ya hasara wanazopata kufuatia vita hivi ambapo wataalam wanaeleza kuwa takwimu zinazotolewa na pande zote mbili haziakisi ukweli kwa kuwa idadi ya vifo hupunguzwa maradufu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW