1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Urusi inavuruga shughuli za usafiri Ukraine

1 Februari 2026

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema Urusi inaendelea kulenga kuvuruga miundombinu ya usafirishaji na mawasiliano kati ya miji na vijiji nchini Ukraine.

Ukraine |
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ahimiza umuhimu wa mifumo zaidi ya anga kwa Ukraine.Picha: Ukrainian Presidential Office/AFP

Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Zelenskiy amesema katika kipindi cha wiki moja pekee, Urusi imetumia zaidi ya droni 980, takribani mabomu 1,100 na makombora mawili dhidi ya Ukraine, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa anga.

Huku haya yakijiri Katibu wa Baraza la Ulinzi wa Taifa nchini Urusi, Sergei Shoigu, amewasili China kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi kuhusu masuala ya usalama wa kimataifa na kikanda.

Ziara hiyo inafanyika sambamba na mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Urusi, Ukraine na maafisa wa Marekani yanayolenga kutafuta njia ya kumaliza vita vinavyoendelea kwa karibu miaka minne.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW