1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky: Wanajeshi 31,000 wa Ukraine wameuawa vitani

26 Februari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema ushindi wa nchi yake "unategemea" uungwaji mkono wa nchi za Magharibi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akitembelea vikosi vyake mjini Kharkiv
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akitembelea vikosi vyake mjini Kharkiv Picha: Ukraine Presidency/Bestimage/IMAGO

Rais Volodymyr Zelensky ameeleza matumaini yake kuwa Marekani itaidhinisha kifurushi cha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.

Zelensky pia amekiri kuwa, wanajeshi 31,000 wa Ukraine wameuawa na kuongeza kwamba Urusi inapanga kufanya mashambulizi zaidi katika msimu wa joto.

Ametoa wito kwa nchi za Magharibi kuiunga mkono Ukraine kwa dhati ili kuipa nafasi ya ushindi katika kumbukumbu ya miaka miwili ya uvamizi wa vikosi vya Urusi.

Katika wiki za hivi karibuni, wanajeshi wa Ukraine wamekabiliwa na uhaba wa risasi na makombora, baada ya mzozo katika bunge la Marekani kuhusu msaada wa kijeshi wa dola bilioni 60 kwa Kiev.

Wiki iliyopita, wanajeshi hao walilazimika kuondoka katika mji wa mashariki wa Avdiivka katika jimbo la Donestk ambako hali inaripotiwa kuwa mbaya.