Zelensky: Wanajeshi wa Urusi warejeshwa nyuma Sumy
13 Juni 2025
Matangazo
Kwenye ujumbe wake kwa njia ya video usiku wa kuamkia leo, Zelensky aliwashukuru wanajeshi kwa kile alichokiita mafanikio yao.
Vikosi vya Urusi vimekuwa vikisonga mbele ndani ya mkoa huo tangu mwezi Aprili, huku Rais Vladimir Putin akitaka lianzishwe eneo lisilo shughuli za kijeshi baada ya wanajeshi wa Ukraine kuondolewa kwenye mkoa wa magharibi mwa Urusi wa Kursk.
Soma zaidi: Pistorius akataa Ujerumani kubadili sera kuelekea Urusi
Pande zote mbili zimethibitisha kuwa Urusi imetwaa vijiji kadhaa vya mkoa wa Sumy, ambao umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na jeshi la anga la Urusi.