1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelenskyy ahimiza kupelekewa silaha haraka

17 Februari 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatolea mwito washirika wa Magharibi kuhakikisha wanazifikisha haraka silaha walizoahidi kuipatia Ukraine.

Deutschland | Münchner Sicherheitskonferenz | Wolodymyr Selenskyj
Picha: Johannes Simon/Getty Images

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa mwito huo na kuonya kwamba iwapo silaha hizo zitachelewa kufika, basi Urusi itafanikiwa katika vita vyake dhidi ya Kyiv. Zelensky ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa wa usalama mjini Munich wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukikaribia mwaka mmoja. Takribani viongozi 40 wa nchi na serikali pamoja na wanasiasa na watalaamu wa usalama kutoka karibu nchi 100, ikiwemo Marekani, Ulaya na China, wanahudhuria mkutano huo wa siku tatu. Kwa mara ya kwanza katika miongo miwili, waandalizi wa kongamano hilo hawakuwaalika maafisa wa Urusi mjini Munich. Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema vita vya Urusi nchini Ukraine vitatawala katika mkutano huo.