1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelenskyy ahimiza silaha zaidi kwa nchi yake

18 Januari 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa mara nyingine amewahimiza washirika wake wa Magharibi kufanya uamuzi wa haraka wa kuipa nchi yake silaha nzitonzito.

Deutschland, Berlin | Diskussion mit Selenskyj an der HU Berlin
Picha: Dmytro Katkov/DW

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa mara nyingine amewahimiza washirika wake wa Magharibi kufanya uamuzi wa haraka wa kuipa nchi yake silaha nzitonzito.

Zelensky amesema anatarajia maamuzi zaidi kufanywa wiki hii katika mikutano miwili: Ile ya Kiuchumi inayoendelea Davos na mkutano mkubwa wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuhusu Ukraine utakaofanyika Ujerumani siku ya Ijumaa.

Katika tukio jingine,

Waokoaji wamesema operesheni yao ya kutafuta manusura au miili kwenye vifusi vya jengo la makaazi ya watu lililoshambuliwa na Urusi mjini Dnipro mwishoni mwa wiki, imekamilika.

Lakini licha ya kumaliza kwa operesheni yao, wamesema watu 20 bado hawajulikani waliko. Watu 39 waliokolewa kwenye vifusi vya jengo hilo.

Maafisa wamesema idadi ya vifo imepanda na kufikia watu 44. Jumla ya watu 79 walijeruhiwa.

Ukraine imesema jengo hilo la ghorofa lilishambuliwa na kombora la Urusi aina ya Kh-22.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW