Zelenskyy asema hayapokea majibu ombi la mkutano na Putin
13 Mei 2025
Zelensky ameyasema hayo kupitia hotuba yake kwa taifa aloitoa usiku wa kuamkia leo. Ofisi yake imesisitiza Zelenskyy anataka kukutana na Rais Putin na siyo wawakilishi wengine wa Urusi, kwenye mazungumzo yaliyopendekezwa na Putin mwenyewe mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hadi sasa Moscow haijasema chochote kuhusu uwezekano wa Putin kukutana na Zelensky siku ya Alhmisi mjini Istanbul. Wakati hayo yakijiri maandalizi ya awali ya mkutano kati ya pande hizo mbili yameanza kwa mazungumzo ya maafisa wa ngazi ya juu.
Hapo jana Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alizungumza na mwenzake wa Uturuki Hakan Fidan huku mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Marco Rubio alifanya mashauriano na mawaziri wenzake wa nchi za Ulaya ikiwemo, Uingereza na Ufaransa.