1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelenskyy kufanya ziara nchini Uingereza

8 Februari 2023

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky atazuru Uingereza leo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini Uingereza tangu Urusi ilipoanza uvamizi wake karibu mwaka mmoja uliopita.

Ukraine | Präsident Selenskyj
Picha: Presidential Office of Ukraine

Aidha, ni ziara yake ya pili pekee iliyothibitishwa ya nje ya Ukraine kufanyika wakati wa vita hivyo vinavyoendelea. Serikali ya Uingereza imesema Zelensky atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu Rishi Sunak, atalihutubia bunge na kukutana na wakuu wa jeshi la Uingezera.

Uingereza ni moja ya nchi zinazoiunga mkono pakubwa Ukraine kijeshi na imetuma nchini humo silaha na vifaa vya kijeshi vya thamani ya zaidi ya pauni bilioni 2.

Ziara hiyo imejiri wakati Sunak akitangaza kuwa Uingereza itawapa mafunzo ya kijeshi marubani wa Ukraine kwa kutumia ndege za kivita za viwango vya Jumuiya ya NATO. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW