1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky atoa wito wa utekelezwaji wa mkataba wa nafaka

18 Julai 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito wa kuendeleza utekelezaji wa mkataba wa usafirishaji wa nafaka katika Bahari Nyeusi licha ya Urusi kujiondo kwenye makubaliano.

Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky atoa taarifa baada ya mazungumzo na mwenzake wa Korea Kusini
Rais wa Ukraine Volodymr ZelenskyPicha: Sergei Supinsky/AFP

Zelensky amesema tayari amewaandikia barua rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres juu ya kuendeleza mpango huo.

Zelensky asema makubaliano yanasalia kuwa halali

Zelensky amesema kuwa mpango wa usafirishaji nafaka katika Bahari Nyeusi unapaswa kuendelea hata bila ya Urusi na kwamba makubaliano ya usafirishaji nafaka ni kati ya Uturuki na Umoja wa Mataifa na yanasalia kuwa halali. 

Urusi adai makubaliano hayatanufaisha mataifa maskini

Makubaliano hayo ya usafirishaji wa nafaka yaliruhusu tani milioni 32.9 za chakula kusafirishwa kutoka Ukraine tangu mwezi Agosti, na zaidi ya nusu yake zilielekea katzika mataifa yanayoendelea. Hata hivyo Urusi imedai kuwa mataifa maskini hasa ya Kiafrika hayakunufaika na makubaliano hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW