1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZIARA YA BUSH BARANI ULAYA

21 Februari 2005

BRUSSELS: ZIARA YA BUSH BARANI ULAYA

Rais George W.Bush wa Marekani amewasili nchini Ubeligiji kwa ziara ya siku nne barani Ulaya. Lengo la ziara hiyo ni kurekebisha uhusiano na washirika wake wa Ulaya baada ya kuwepo maoni tofauti kuhusu Iraq na masuala mengine.Hatua kali za ulinzi zimechukuliwa mjini Brussels ambako leo hii Bush atakuwa na majadiliano pamoja na viongozi wa Ubeligiji kabla ya kuelekea Ufaransa kwa chakula cha jioni pamoja na rais Jacques Chirac.Bush siku ya jumanne atakutana na viongozi wa Shirika la Kujihami la Magharibi-NATO na wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels.Siku ya jumatano ziara yake itamfikisha Ujerumani kwa mazungumzo na Kansela Gerhard Schroeder mjini Mainz.Hatimae Bush ataelekea Slovakia kukutana na rais Vladimir Putin wa Russia.Watu kwa maelfu wanatazamiwa kufanya maandamano wakati wa ziara ya Bush,ambayo ni ziara yake ya mwanzo ya kigeni tangu kushika madaraka mwezi uliopita kwa kipindi cha pili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW