1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZIARA YA KANZELA SCHRÖDER WASHINGTON NA KURA YA IMANI BUNGENI NDIO MADA KUU ZA WAHARIRI

28 Juni 2005

Tukianza na ziara ya Kanzela Schröder kwa rais Bush,mjini Washington, gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung laandika:

“Inadhihirika kuwa Bw.Schröder ameahidi huko kuwa Umoja wa ulaya katika mazungumzo na Iran juu ya (mradi wake wa kinuklia) itaitia shinikizo na pia ameonya kugutuka haraka kuiwekea vikwazo.Yabainika Schröder anaamini kuwa utawala wa Bush kudhibitiwa mamlaka nchini Iran na wafuasi wenye itikadi kali,kunamfungulia mlango rais Bush kufuata mkondo wa siasa zake za mpambano na Iran……….Onyo alilotoa Schrödfer ni kuungama kwake kwamba halikuwamo katika kifurushi alichokwenda nacho Washington.

Kwa upande mwengine,haiwezi kutarajiwa kwamba Schröder nae angeagwa kwa kupewa zawadi ya kumsaidia katika uchaguzi ujao:Marekani kuihakikishia Ujerumani kupata kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la UM.”

DIE WELT nalo linasalia katika mada hii hii likiandika kwamba, Kanzela Schröder amepatwa na mapigo 2 mjini Washington:Kwanza , wamarekani wakati huu wanashughulishwa na mada nyengine kabisa kuliko Ulaya……Kun’gan’gania kwa Bw.Scxhröder kudai kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama hakujasaidia kitu na hasa kwavile wajerumani hadi sasa wameshindwa kujieleza kwanini wanataka kiti cha kudumu na siasa zao zitakuaje wwakikalia kiti hicho.Schröder anataka kiti hicho kama ni fahari tu kwa nchi yake ……..

Si ajabu kwahivyo chini ya hali hii, Schröder anarudi Berlin mikono mitupu.” Ni maoni ya DIE WELT.

Ama gazeti la GENERAL-ANZEIGER likimurika siasa za CDU/CSU na Marekani laandika:

Ziara ya Bw.Schröder mjini Washington pengine ni ya mwisho kama Kanzela. Upinzani wa CDU/CSU nao hausemi mengi zaidi ya kutaka kuupalilia urafiki na Marekani katika siasa zao za nje.Utajikuita nao unavutana na utawala wa Bush.Kwani, hodi hodi za mwanachama wa NATO Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya, haziitikiwi na wingi wa wanachama wa CDU/CSU.Na kwa azma yake mwenyekiti wa CDU Bibi Angela Merkel kutozuru Marekani wakati wa kampeni ya uchaguzi na kungoja kwanza kushika madaraka ya siasa za nje,si uamuzi wa busara.

Ama gazeti la OSTSEE ZEITUNG litugeuzia mada likichambua uamuzi wa Kanzela Schröder wa kupigiwa kura ya imani Bungeni:

Kwa sentensi 2 alizomuandikia rais wa Ujerumani,Kanzela Schröder amefungua jana mlango wa kuaga kwake jukwaa la kisiasa.Anataka kupitia kura ya kutokua na imani nae Bungeni,paitishwe uchaguzi mpya.Mwiba mchongoma ni kuwa hakuweza kumyakinisha yeyote kwanini mtu aje kumchagua tena Kanzela ambae Bunge lilipiga kura ya kutokua na imani nae……

Gazeti la ABENDZEITUNG litokalo Munich laandika :

“Kanzela bado ana wingi wa kura Bungeni sawa na pale alipochaguliwa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.Kwamba,Bw.Schröder hivi sasa amechoshwa na kazi yake,inaweza kufahamika,lakini kuna chombo cha kutumia kuonesha uchofu huo:kujiuzulu madarakani.Njia lakini aliyoichagua Bw.Schröder ya kupigiwa kura ya imani ni ukiukaji dhahiri- wa katiba.”

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW