1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya kwanza ya kiongozi wa Venezuela yafutwa ghafla

13 Machi 2026

Ziara ya kwanza ya kigeni ya kiongozi wa mpito wa Venezuela anayoungwa mkono na Marekani tangu Delcy Rodríguez imeghairishwa ghafla, saa chache kabla ya kuwasili Colombia.

Venezuela Caracas 2026 | Rais wa Muda Delcy Rodríguez katika ufunguzi wa mwaka mpya wa mahakama
Delcy Rodríguez, kiongozi wa mpito wa VenezuelaPicha: Miraflores Palace/REUTERS

Ziara ya kwanza ya kigeni ya kiongozi wa mpito wa Venezuela anayoungwa mkono na Marekani Delcy Rodríguez imeghairishwa ghafla, saa chache kabla ya kuwasili Colombia. Rodríguez alitarajiwa kusafiri hadi mji wa mpakani wa Cúcuta kwa ajili ya mkutano wa kilele leo Ijumaa na Rais wa Colombia, Gustavo Petro.

Haikufahamika mara moja ni kwa nini safari hiyo imefutwa, ingawa chanzo kimoja upande wa Colombia kimeelezea kuwepo kwa ripoti za kitisho cha usalama, bila kufafanua ikiwa ni upande wa Venezuela au Colombia.

Eneo linalozunguka Cúcuta lina makundi mengi ya waasi wa mrengo wa kushoto yanayojihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya ambayo Colombia imekuwa ikiituhumu Venezuela kwa kuyafadhili kwa muda mrefu. Rodríguez aliingia madarakni Januari baada ya Nicolas Maduro kukamatwa na Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW