1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Rais Bush barani Ulaya

18 Februari 2005

Washington:

Rais wa Marekani, George W. Bush, ataitumia ziara yake ya juma lijalo kuziba tofauti zilizopo kati ya nchi yake na Ulaya. Atatoa mwito wa kuungana baada ya uchaguzi mkuu wa Irak na kuwaomba Washirika wake wazidi kuzishinikiza Iran na Siria. Rais Bush amesema kuwa lengo kubwa la ziara yake itakayoanza Jumapili ni kuwakumbusha Wamarekani na Wazungu kuwa ushirikiano uliopo kati yao ni muhimu sana kwa ajili ya usalama wao na amani. Ingawaje wakati mwingine tofauti hutokea lakini hawatofautiani kiuadilifu. Rais Bush amesema kuwa atawaambia Wananchi wa Ulaya kuwa Marekani inahusika pia na mabadiliko ya hali ya hewa na inataka kuwe na ushirikiano wa kuendeleza teknolojia za kupambana na hali hiyo. Rais Bush atakutana na Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya na Shirika la Kujihami la Magharibi (NATO) mjini Brussels, Ubelegiji. Atakutana na Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani mjini Mainz na atazungumza pia na Rais Vladimir Putin wa Urussi mjini Bratislava, Slovakia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW