1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Köhler atembelea Kano na Lagos.

Mtullya, Abdu Said11 Novemba 2008

Rais wa Ujerumani Horst Köhler aendelea na ziara nchini Nigeria.

Rais Horst Köhler wa Ujerumani na rais Umaru Yar Adua wa Nigeria.Picha: picture alliance -dpa


Rais wa Ujerumani Horst Köhler anaendelea na ziara nchini Nigeria ametembelea mji wa Lagos na jimbo la Kano.

Rais Köhler ambae tayari amefanya mazungumzo na rais Yar Adua wa Nigeria amesema ni muhimu kwa Nigeria kupeleka maendeleo katika sehemu za mashambani vilevile.

Ameeleza kuwa ili kufikia shabaha hiyo pana haja ya kuendeleza miundombinu itakayowawezesha wakulima wadogo wadogo kufikisha mazao yao sokoni. Amesema ni kwa njia hiyo tu kwamba itawezekana kupambana na umasikini kwa ufanisi nchini Nigeria.

Kiongozi huyo wa Ujerumani anaefanya ziara ya nne barani Afrika pia ameitaka jumuiya ya kimataifa isaidie katika harakati za kupambana na rushwa inayosababisha utajiri wa Nigeria kushindwa kuwanufaisha watu wake wengi.

Rais huyo ameshauri kuwekwa kwa utaratibu utakaozuia wizi wa mafuta ya Nigeria.




Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW