Ziara ya rais Köhler Msumbiji
4 Aprili 2006Rais Horst Köhler wa Ujerumani akiendelea leo na siku yake ya pili ya ziara yake nchini Msumbiji,anakutana na rais wa zamani wa Afrika kusini,mzee Nelson Mandela.Mwanzoni kabisa wa mwa ziara yake alipongeza juhudi za kimaendeleo ilizofanya Msumbiji kuwa ni za kupigiwa mfano.
Licha ya kuipongeza Msumbiji kwa juhudi zake za kimaendeleo, rais Köhler alisema mengi bado yanabidi kufanywa humo nchini ,mfano kupiga vita rushua.Msumbiji ambayo bado inaathirika na umasikini na ukosefu wa watu wake wengi bado kutojua kusoma na kuandika,imekua tangu kumalizika vita vya kienyeji vya miaka 16, hapo 1992 ,ikifuata mkondo wa kidemokrasia.
Hii ni ziara ya kwanza ya rais wa ujerumani nchini Msumbiji.Hatahivyo, rais Köhler akiijua Msumbiji wakati alipokuwa Mkurugenzk wa Shirika la Fedha Ulimwenguni.
Tayari wakati wa ziara zake wakati ule 2002 na tena 2003,aliona Msumbiji kuwa ni nchi iliofuata mkondo wa mageuzi.Alieleza msumbiji hata wakati wa ziara yake hii ya sasa kuwa Msumbiji , ni nchi ya kupigiwa mfanmo.
Hatahivyo, Msumbiji imetoka mbali:Pale vita vya kienyeji vilipomalizika 1992 baada ya miaka 16, miundo-mbinu ya nchi hii ilikuwa imeteketezwa kwa vita.Shule zilibomoka na wananchi walikuwa tafrani .
Leo hii lakini, Msumbiji ni mojawapo ya nchi zinazopiga hatua haraka kabisa kiuchumi barani Afrika. Hatahivyo, katika sekta za kuukuza uchumi,maendeleo ya vijijini na elimu, Jule Riviere,anaeongoza misaada ya maendeleo ya Ujerumani humo nchini anaeleza hivi :
“Kwa kweli, nchi hii inakabiliwa na changamoto kubwa., kwani mashule mengi yaliharibiwa na vita vya kienyeji,walimu wengi wanaugua maradhi ya UKIMWI na kwa kuwa watoto wengi hata shule hawendi.”
Msumbiji imenyosha njia barabara na ni azma ya rais Köhler katika ziara hii kubainisha hayo wazi.Hata Kiongozi wa afisi ya Banki ya mikopo kwa ujenzi upya mjini Maputo,Carsten Sandhop,anajionea pia maendeleo iliopiga nchi hii. Anataja pia sekta ambazo anahisi mengi zaidi yanastahiki kufanywa kuliko ilivyofanyika hadi sasa:
“Masharti yaliokuwapo nchini Msumbiji yalikuwa zaidi magumu.Vita vya kienyeji vilikwishamalizika miaka 16 nyuma,lakini viliteketeza kwa kadri kubwa miundo-mbinu iliosimamisha maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi.
hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 ulichangia pia.Hata hatua za mageuzi ilizochukua Msumbiji hazikupita bila upinzani na kutiwa munda.
Ushahidi wake unaonekana katika kashfa kadhaa zilizofungamana na miradi ya ubinafsishaji wa mashirika ya serikali.Ushahidi mwengine ni kuwa hakuna viwanda vya wastani vilivyotia raslimali zao nchini Msumbiji kwavile hakujakuwa na masharti ya kuvutia raslimali kama hizo.”-asema Carsten Sandhop.
Kwahivyo, ukosefu wa sheria za kulinda raslimali na rushua kulizuwia maendeleo ya haraka kwa msumbiji.Pingamizi nyengine ni kwa Msumbiji tangu zaidi ya miongo 3 chama kile kile -FRELIMO- kimen’gan’gania madaraka na Upinzani hauna sauti yoyote.Hii imeongoza kuwapo tabaka maalumu ya aina ya wakereketwa wanaotia munda mageuzi.
Hata swali hili amepanga rais Köhler kulizungumzia na viongozi wa kisiasa wa Msumbiji wakati wa ziara yake hii.
Hatahivyo, Msumbiji imefanya maendeleo makubwa,kwani mnamo miaka michache tu imefaulu kupunguza kima cha umasikini kutoka 70% na kuwa 54%.Idadi ya watoto wanaoingia mashuleni imepanda mno hadi 50%.Maendeleo hayo yamechangiwa na misaada kutoka nchi za nje.Kwani, nusu ya bajeti ya msumbiji inagharimiwa na misaada ya fedha za wafadhili.
Ujerumani imeongeza mwaka jana mara tatu msaada wake kwa Msumbiji na kwa jumla ya Euro Mil. 67 ikikidhi kwa mwaka jana na huu wa 2006,gharama za elimu,uchumi na maendeleo ya vijijini.
Baada ya kuondoka Msumbiji,rais wa Ujerumani anapanga kuzuru Madagaskar na Botswana.