1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZIARA YA RAIS PUTIN UJERUMANI NA MKASA WA KATIBU-MKUU WA CDU NDIO MADA GAZETINI LEO:

22 Desemba 2004

Gazeti la FINANCIAL TIMES LA UJERUMANI kuhusu mazungumzo kati ya kanzela Schröder na mgeni wake rais Putin wa Russia:

"Ulikua mkutano uliokwenda kwa ladha ya Schröder.Kwani, magari-moshi yatakayosafiri kati ya mji wa Moscow na St.Petersberg,yataundwa na kampuni la SIEMENS la Ujerumani.Russia italipa madeni yake kwa ujerumani.Mzozo kuhusu Ukrain umeshasahauliwa.

Viongozi wa dola wanakuja na kwenda zao,lakini umma wa Ukrain upo pale pale-ndio hukumu ya hivi punde aliotoa rais wa Russia kuhusu mapinduzi mjini Kiev.Hgata kilio cha ujerumani cha kujipatia kiti cha kudumu katika baraza la Usalama lka UM –Urusi inakiungamkono.

Kwahivyo, Kanzela Schröder,amethibitishiwa mkondo wake wa siasa mbele ya Russsia ni barabara.Matokeo ya mazungumzo kati ya Schröder na Putin katika Qasri la Gottorf yameongoza hata katika maafikiano kwamba kuanzia sasa hata katika mada ya Chechnia,haifai tena kufumba mdomo."-hilo lilikua FINANCIAL TIMES.

Msimamo huu umechukuliwa pia na gazeti la DIE WELT.Laandika je, Kanzela Schröder akieleza hapo hekaya za kale za kirusi za X-masi,au kweli rais Putin ana azma ya kufungua ukurasa mpya wa siasa zake kuutatua mgogoro wa Chechnia ?

Ni mapema kuamua iwapo ahadi za Putin ni kweli au ni mchezo wa kidiplomasia.Chechnia haiwezi kusonga mbele ikiwa kila kukicha ugaidi unapaliliwa.Na hii si kwa masilahi ya rais Putin.labda sasa nae amen’gamua kwamba Russia haiwezi pekee kulitatua tatizo la Chechnia.Mchango gani Ujerumani inaweza kutoa kufumbua kitandawili hicho kamanavyodai Schröder,haifahamiki."Hayo ni maoni ya DIE WELT.

Ama gazeti la kibiashara-HANDELSBLATT likin’Ägan’ngania nalo mada hii hii laandika:

"Mara kwa mara anapozuru Ujerumani,rais Putin amekuwa akisema ameweka sikio wazi kwa mashauri jinsi ya kukifumbua kitandawili cha Chechnia kwa njia za kisiasa.Kusema hivyo ni kuungama kwamba mambo yanamuendea kombo na wakati huo huo ni changamoto.Putin anakiri hapo kwamba siasa yake kuelekea Chechnia,imepanda mwamba.Wakati huo huo anatoa changamoto kwa wanaomkosoa huku magharibi wajitwike nao dhamana ya kuutatua mzozo huo.Kwa kujitolea sasa mazungumzo kuutatua mzozo wa Chechnia ,amepiga hatua ya kwanza."

Tukiligeukia gazeti la TAGESSPIEGEL nalo lasema kwamba, Kanzela Schröder anaamini barabara aegemee uzi ule ule.Putin kama yeye Schröder, wametoka hali ya chini na kupanda kileleni mwa madaraka.Isitoshe,Putin ni kiongozi pekee wa dola ambae Schröder aweza kuzungumza nae bila kuhitaji mkalimani,kwavile Putin azungumza kijerumani barabara.Kwahivyo, ni wazi kabisa,Schröder anachelea kumkosoa Putin hadharani juu ya sera zake kuelekea Chechnia.Pia amekueleza kusambaratishwa kwa kampuni la mafuta la JUKOS ni mzozo wa ndani wa Russia....

Likitubadilishia mada, gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG lachambua matamshi ya Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani Bibi Angela Merkel juu ya mkasa wa Katibu mkuu wa chama Laurenz Meyer Gazeti laandika:

"Hii ni habari nzuri:katibu mkuu wa CDU hakufanya madhambi yoyote.Amelipa kodi kutoka fedha zote alizovuna..... na eti sasa Bw.-Meyer ametambua ilikuaje hakuelewa kwanini wakati ule alipokea hizo fedha.Na hasa swali hili ndilo lililoeleweka wazi.Ilikuaje akapewa fedha hizo ndio vigumu kufahamika."Laandika FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG.

Mwishoe,tumalizie kwa uchambuzi wa gazeti la KÖLNER STADT-ANZEIGER:Nalo laandika juu ya mkasa huu:

"Katibu-mkuu wa CDU Laurenz Meyer alijijuvya barabara juu ya mkasa huu na ilikuaje akalipwa kiinuamgongo kilichonona kutoka shirika la RWE.Lakini hakikua kiinua-mgongo-si chini ya sheria za kazi wala kwa tafsiri halisi ya neno hilo.Kwahivyo mtu aweza tu kukisia :kwa kazi gani mbunge Meyer alipokea malipo hayo maalumu kutoka kampuni hilo-nayo kampuni hilo lilikitaka kuwa na usuhuba mwema na wanasiasa."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW