1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Sharaa Marekani ni mpango mpya wa kikanda?

13 Novemba 2025

Syria ilijiunga na kundi linaloongozwa na Marekani la mataifa yanayopambana dhidi ya kundi la "Dola ya Kiislamu”, hatua hii ya Syria ina umuhimu mkubwa zaidi katika kujipanga upya kwa wahusika katika mapambano hayo.

Marekani, Washington  2025 | Donald Trump na Ahmed al-Sharaa
Rais wa Marekani Donald Trump akimkaribisha mwenzake wa Syria Ahmed al-SharaaPicha: SANA/AFP

Kiongozi wa mpito wa Syria Ahmad al-Sharaa ambaye aliwahi kuwa mpiganaji katika kundi la al- Qaeda na kufungwa Marekani kama gaidi wiki hii alikaribishwa katika Ikulu ya White House na rais Donald Trump.

Mwanachama huyo wa zamani wa Al-Qeada alisaini mkataba wa nchi yake kujiunga na muungano wa kimataifa kupambana na kundi la wapiganaji wa itikali kali linalojiita "Dola la Kiislamu” IS ambalo liliwahi kuwa mshirika wa  Al- Qaeda nchini Iraq.

Kundi  la wapiganaji la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) lililojitenga na Al-Qaeda mwaka 2016,liliongozwa na Al Sharaa  kuuondowa utawala wa kidikteta wa Bashar Al- Assad nchini Syria. Baadaye  kundi hilo lilipigana dhidi ya  IS kwa miaka kadhaa ndani ya Syria.

Ama baada ya kujiunga kama mwanachama wa 90 wa muungano huo dhidi ya IS, Syria imejiweka katika ngazi ya juu katika mapambano hayo ikikumbukwa kuwa IS ingali na ushawishi miongoni mwa raia wa Syria.

Kulingana na wachunguzi IS ina wafuasi takriban 3,000 nchini Syria na hivi karibuni imekuwa ikiwasajili hasa wale waliokuwa wafuasi wa Assad kujiunga na kundi hilo.

Serikali ya Syria sasa inatakiwa kuimarisha zaidi ushirikiano wake na kundi la Wakurdi la Syria Defence SDF Forces lenye ngome zake Kaskazini mwa nchi hiyo na ambalo limekuwa likifadhiliwa na Marekani katika kushiriki mapambano dhidi ya IS.

SDF ambayo imekuwa ikipambana dhidi ya IS kati ya mwaka 2014 na 2019 inawashikilia zaidi ya  wafuasi 45,000 wa IS katika kambi kadhaa wakiwa na familia zao.

Wachambuzi: IS hujiimarisha katika mizozo

Kulingana na Tanya Mehra ambaye ni mtafiti katika Kituo cha Kimataifa cha kupambana na Ugaid ICCT chenye makao yake Uholanzi, IS hujiimarisha katika mazingira ya mizozo na ndiyo maana walistawi wakati wa vita vya Syria na hata kabla ya utawala wa Syria kudhibiti hali waliendelea na harakati zao.

Mwanamume akiwa ameshikilia bendera za Marekani na SyriaPicha: Brendan Smialowski/AFP

Mwishoni mwa wiki vikosi vya usalama vya Syria viliendesha operesheni sehemu mbalimbali za nchi hiyo na kuwakamata watu 71 wanaoshukiwa kuwa na mafungamano na IS.

Ripoti zinaonesha kuwa sehemu ya mafanikio yametokana na taarifa zilizotolewa na Marekani.

Hii ina maana kuwa Syria tayari imekuwa ikishirikiana na Marekani hata kabla ya kujiunga na muungano huo wa kimataifa.

Makubaliano ya kuanzishwa kwa kituo cha kijeshi

Lakini kwa mujibu wa wataalamu matokeo makubwa ya Syria kujiunga na muungano huo wa Marekani ni makubaliano kati yake na Washingtonn kuanzisha kituo cha kijeshi cha Marekani jirani na mji wa Damascus.

Kwa mujibu wa habari ambazo hazijathibitishwa, wiki iliyopita, takriban wajumbe 80 kutoka muungano huo walitembelea kituo cha jeshi la anga cha Al-Seen kilicho umbali wa kilomita 80 kutoka Damascus.

Wadadisi wanaelezea kuwa ikiwa Marekani itaanzisha kituo hicho, itahitaji kuihakikishia usalama Israel lakini pia kupunguza ushawishi wa mataifa ya Urusi, Iran na Uturuki nchini Syria.

Mzozo wa Sweida na sura zake kijamii, kisiasa na kimataifa

11:48

This browser does not support the video element.

Kulingana na March Lynch ambaye ni profesa wa masuala ya kisiasa na sera za kimataifa, hatua hiyo itatikisa mahusiano Ya Marekani na washirika wake hasa Israel.

Israel imejtenga kabisa na juhudi zinazongozwa na Marekani katika kuijenga tena na kurejesha uthabiti Syria.

Kulingana na Mdadisi mmoja, ikiwa Marekani itaanzisha kituo cha jeshi la anga Damascus, basi ijiandae kuhatarisha  usalama wa Israel  na kwa hiyo kusababisha msuguano wa kisiasa na kidiplomasia na taifa hilo mshirika wake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW