ZILAZALA YAUA SI CHINI YA 270 IRAN
22 Februari 2005Matangazo
KERMAN,IRAN:
Zaidi ya watu 270 wameuwawa na zaidi ya 1000 wamejeruhiwa katika zilzala kali ilioipiga Iran alfajiri ya leo .Wakuu nchini Iran wameonya kuwa idadi ya waliofariki yaweza ikapanda mno kwavile mvua na njia zilizozingwa na maporomoko inatatiza kuvifikia vijiji vyengine vya milimani.
Gavana wa jimbo ambako zilzala hii imwepiga Mohammad Ali Karimi amesema si chini ya watu 270 wamepoteza maisha yao na wengi waliouwawa ni kutoka eneo la Zarand lililoathrika vibnaya sana.
Mtetemeko huu wa ardhi una kipimo cha 6.4 cha Richter.
Nchi jirani ya Uturuki ambayo kama Iran imekuwa ikikumbwa na zilzala mara kwa mara imejitolea kuipa msaada Iran.Iran lakini imekataa msaada huo-kwa muujibu wa waziri mkuu wa uturuki Tayyip Erdogan.