1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZIMBABWE INA NAFASI YAKE KATIKA COMMONWEALTH:

10 Desemba 2003
LONDON: Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema,daima katika Jumuiya ya Madola-Commonwealth,kutakuwepo nafasi kwa Zimbabwe yenye mfumo wa kidemokrasia-lakini kwa hivi sasa itaendelea kutengwa mpaka kutakapokuwepo ishara dhahiri za mageuzi nchini humo.Blair akizungumza bungeni mjini London,katika tangazo lake la mwanzo hadhrani tangu kumalizika mkutano wa Commonwealth nchini Nigeria amesema "Zimbabwe imerudi nyuma."Siasa za kiuchumi za chama cha ZANU-PF zilizo haribifu,zinazidi kuitumbukiza Zimbabwe katika hali ya vurugu aliongezea waziri mkuu Blair.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW