1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe yaomba msaada wa kimataifa kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Kabogo Grace Patricla4 Desemba 2008

Kufikia sasa karibu watu 600 wamefariki kufuatia ugonjwa wa kipindupindu nchini Zimbabwe na kusababisha nchi hiyo kuomba msaada wa kimataifa.

Wanawake na watoto wakisubiri kuchota maji kwenye kisima kutokana na uhaba wa maji nchini Zimbabwe.Picha: AP

Zimbabwe sasa inaomba msaada wa kimataifa ili kukabiliana na kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu ambao kufikia sasa umesababisha vifo vya karibu watu 600. Haya yanajiri huku wanajeshi 16 nchini humo wakizuiliwa kutokana na ghasia za hivi majuzi na uporaji katika maduka ya ubadilishaji pesa za kigeni.



Ugonjwa huo wa kipindupindu ni changamoto ya hivi punde kuikabili zimbabwe; ambayo tayari uchumi wake umezorota kwa kiasi kikubwa na wenyeji kukabiliwa mzozo wa kiutu.

Zaidi ya wa nusu ya idadi ya wazimbabwe wanahitaji kwa dharura msaada wa chakula na hospitali zote za serikali zimefungwa kwa mwezi mmoja sasa kufuatia mgomo wa wadaktari na wauuguzi wakilalamikia mishahara duni na mazingira mabaya ya kufanyia kazi.

Waziri wa afya nchini zimambwe alinukuliwa na gazeti linalomilikiwa na serikali la The Herald akisema hakuna chochote kinachoendelea katika karibu hospitali zote nchini zimbabwe,wafanyikazi wote wamekosa motisha na tunahitaji msaada wa kimataifa ili kuifufua tena secta ya afya.

Wataalam wa mambo ya afya wameishtumu serikali kutokana na kuzuka kwa ugonjwa huo wa kipindupindu, wakidai serikali ya zimbabwe ilikosa kununua kutoka nje kemikali za kusafisha maji tangu mwezi agosti huu.

Mji wa harare umekabiliwa na uhaba mkubwa wa maji na hivyo kuwafanya wenyeji wake kunywa maji machafu kutoka visima au mito.Afisi ya umoja wa mataifa kuhusu mzozo wa kiutu inakisia kuwa huenda karibu watu 600 wamefariki huku maafa makubwa yakitokea katika mji mkuu harare.

Ugonjwa huo wa kipindupindu tayari umeenea katika taifa jirani na Zimbabwe la afrika kusini ,ambapo watu saba wamefariki katika mpaka wa mji wa musina.

Wakosoaji pia wamesema matatizo yanayoendelea nchini Zimbabwe yametokana na sera mbovu za uongozi za rais Robert Mugabe na hali hata imekuwa mbaya zaidi kutokana na mkwamo wa kugawana nyadhifa za uwaziri kati yake na upinzani.

Waziri wa maji na miundo msingi Walter Nzembi amesema wizara yake ina chemikali za kusafisha maji zitakazo dumu kwa wiki 12 pekee. Waziri huyo ameomba msaada wa dolla millioni 3.89 kutoka kwa wafadhili ili kuweza kununua kemikali hizo msaada anaouhitaji kati ya leo na jumatatu ijayo.Serikali ya zimbabwe pia imeomba msaada wa dolla millioni 450 kukabiliana na uhaba wa chakula nchini humo.

Huku hayo yakijiri wanajeshi 16 nchini humo wanazuiliwa kutokana na ghasia za hivi majuzi za uporoji katika maduka ya ubadilishanaji fedha za kigeni, mjini harare. Inadaiwa wanajeshi hao sita walikuwa miongoni mwa wengine 10 wanaliowapiga raia na kushiriki uporaji.

Wanajeshi hao walikuwa wakifanya msako mjini harare katika harakati za kuwatia mbaroni wafanyibiashara wanaoendesha bishara hiyo kimagendo.Wachanganuzi wamesema kisa hicho kinadhihirisha kuendelea kuzorota kwa hali ya uchumi na matatizo yanayoikabili serikali ya rais Mugabe.


Serikali ilikuwa imeapa kuwachukulia hatua wanajeshi waliohusika.


►◄




Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW