Zimbabwe yaondoa hukumu ya kifo
2 Januari 2025Rais Emmerson Mnangagwa aliyewahi kupewa hukumu ya kifo katika miaka ya 60 katika vita vya kuwania uhuru wa taifa hilo, alipitisha sheria hiyo wiki hii baada ya msuada wa kuondoa hukumu hiyo kupitishwa bungeni.
Zimbabawe ina wafungwa 60 waliotakiwa kupewa hukumu hiyo lakini wamenusurika kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo mpya inayoondoa adhabu hiyo. Mara ya mwisho Zimbabwe kutoa hukumu ya kifo ilikuwa mwaka 2005.
Soma pia: Watu 37 wahukumiwa kifo kwa jaribio la mapinduzi DRC
Shirika la kutetea haki zabinaadamu la Amnesty International limepongeza hatua ya hukumu ya kifo kufutiliwa mbali Zimbabwe likisema inatoa matumaini ya kuondoa kabisa hukumu hiyo katika kanda nzima.
Mataifa mengine ya Afrika kama Kenya, Liberia na Ghana hivi karibuni zimechukua hatua muhimu kuondoa hukumu hiyo lakini bado haijaliweka hilo rasmi kisheria.