1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe yawalilia wafadhili na wakopeshaji wa kimataifa

4 Mei 2020

Waziri wa fedha wa Zimbabawe Mthuli Nbube amesema nchi hiyo inaelekea kutumbukia kwenye janga kubwa la kiafya na kiuchumi kutokana na mripuko wa virusi vya Corona kutokana na mzigo wake wa madeni.

Simbabwe | Medizinische Angestellte bereiten sich auf mögliche Corona-Fälle vor
Picha: Reuters/P. Bulawayo

Waziri huyo amesema katika barua iliyoandikwa Aprili pili iliyolifikia shirika la habari la Reuters leo Jumatatu kwamba Zimbabwe inahitaji kuanza mazungumzo na kurudisha uhusiano wa kawaida na wakopeshaji wakigeni ili  kuyamaliza malimbikizo yake ya madeni ya miongo kadhaa na kufungua fursa ya kupata fedha za haraka zinazohitajika.

Ncube ameleeza kwenye barua yake kwamba maofisa nchini Zimbabwe wanapendekeza uwepo mdahalo wa ngazi ya juu  kuhusu kuzuia hali mbaya zaidi ya kiuchumi na kijamii kutokea nchini humo kufuatia janga la ugonjwa wa Covid-19.

Barua hiyo imetumwa kwa shirika la fedha la kimataifa IMF na benki ya dunia pamoja na benki ya maendeleo ya Afrika,benki ya uwekezaji ya Ulaya miongoni mwa taasisi nyingine za fedha.Wakopeshaji kama IMF na benki ya dunia zilisita kuipa mkiopo Zimbabwe mwaka 1999 baada ya nchi hiyo kushindwa kurudisha mkopo huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW