1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe yazindua noti mpya

28 Novemba 2016

Zimbabwe imetangaza kuanza kutumia noti mpya, ikitoa noti ya dhamana za serikali ya dola milioni 10, ambazo zinatazamiwa kusaidia kupunguza matatizo makubwa ya upatikanaji wa fedha.

Protest Harare Simbabwe
Picha: DW/P.Musvanhiri 

Matatizo ya kifedha yaliikumba nchi hiyo iliyo Kusini mwa Afrika na kupelekea kutumia fedha mbalimbali za nje ikiwemo dola ya Marekani tangu mwaka 2009; baada ya kiwango cha mfumko kufikia kilele chake kwa asilimia bilioni 500 na kusasabisha dola ya Zimbambwe kutokutumika.

Kutambulishwa kwa noti za dhamana za dola 2 na 5 katika mzunguko wa fedha kunafuatia pia kutambulishwa kwa sarafu ambazo zilianza kutumika mwaka mmoja uliopita ili kupunguza upungufu wa ubadilishaji fedha.

Zimbabwe imekumbwa na uhaba mkubwa wa dola ya Marekani katika miezi ya hivi karibuni, hali ambayo ilipelekea serikali ya raisi Robert Mugabe kuchapisha fedha ambayo imepewa jina la utani la fedha mbadala.

Wananchi wanapinga kutambulishwa kwa noti hizo mpya kwa sababu bado wanahasira na kuanguka kwa dola ya Zimbabwe, ambayo ilitelekezwa mwaka 2009, kutokana na mfumuko mkubwa wa bei anasema mhariri wa gazeti huru la wiki, the standard, na kuongeza kuwa serikali imekuwa na kiburi,na kuwatawanya wale ambao wamekuwa wakipinga fedha mbadala na kuonekana kuwa si wazalendo.

Waandamanaji wakipinga utambulisho wa noti mpya nchini ZimbabwePicha: picture-alliance/AP Photo/T. Mukwazhi

Utoaji fedha katika banki wadhibitiwa

Benki kuu nchini humo imefanya uzinduzi wa matangazo katika vyombo vya habari kujaribu kuwatisha watu na kusema kuwa wafanya biashara wadogo na wakubwa wamekubali utambulisho wa noti hizo, japo utambulisho wa noti hizo umezusha hofu ya upungufu wa mafuta katika vituo kwa wiki iliyopita na kusababisha msongamano mkubwa katika vituo vya kuuza mafuta.

Serikali kwa upande wake, imewataka madereva kutokuwa na wasiwasi na kusema kuwa kuna mafuta ya kutosha yamehifadhiwa, katika taarifa iliyotolewa wiki iliyopita serikali imesema "tunapenda kuwahakikishia kuwa nchi hakuna ukweli wowote wa madai kuwa nchi itakumbwa na uhaba wa mafuta"

Utoaji wa fedha banki unadhibitiwa ambapo sasa watumiaji wanaweza kutoa pesa kiwango cha juu cha dola 150 tu kwa wiki.

Uchumi wa nchi hiyo umeaanguka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni huku banki zikikumbwa na uhaba wa fedha hali ambayo iliwachanganya watumiaji wa huduma hizo na kuwalazimisha wengine kulala nje ya banki wakitaka kutoa pesa zao.

Utambulisho wa noti hizo umeamsha hasira ambazo zimesababisha kuibuka kwa waandamanaji mitaani, katika kipindi cha wiki mbili wanaharakati kadhaa walikamatwa na kupigwa kabla ya kufanyika kwa maandamano yaliyopangwa ili kupinga utambulisho wa noti hizo.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW