1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe

Hamidou, Oumilkher11 Oktoba 2008

Rais Mugabe awakabidhi wafuasi wa chama chake nyadhifa muhimu serikali

Harare:

Kwa mujibu wa gazeti la serikali ya Zimbabwe,rais Robert Mugabe amewakabidhi wafuasi wa chama chake nyadhifa muhimu za serikali,bila ya ridhaa ya aupande wa upinzani.Msemaji wa upande wa upinzani ameukosoa uamuzi huo wa upande mmoja akisema unatia hatarini makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa taifa."Ni kiburi hicho cha chama cha ZANU-PF na MDC haitaidhinisha oridha hiyo ya mawaziri" amesema Nelson Chamisa,ambae ni msemaji wa chama cha upinzani cha MDC kinachoongozwa na Morgen Tsvangirai.Chama tawala cha Zanu -PF na upande wa upinzani,wametia saini makubaliano ya kihistoria ya kugawana madaraka september 15 iliyopita.Karibu mwezi mmoja baadae,pande hizo mbili zimeshindwa kukubaliana juu ya kugawana nyadhifa muhimu za serikali ya umoja wa taifa.Pande hizo mbili zimetoa mwito mpatanishi wa mzozo wa Zimbabwe Thabo Mbeki aingilie kati tena.