1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Kandanda

Bado siku 100 kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia

3 Machi 2026

Zikiwa zimesalia siku 100 kabla michuano ya kombe la dunia la kandanda 2026 nchini Marekani, Mexico na Canada, ununuaji wa tiketi umefikia kiwango cha juu mno, huku mashabiki wakilalamikia bei ghali za tiketi hizo.

Canada, Marekani na Mexico, zitashirikiana kuwa wenyeji wa kombe la dunia 2026
Kombe la Dunia litafanyika mwezi Juni 2026Picha: Ulises Ruiz/AFP

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limesema tiketi milioni mbili zimeshauzwa katika awamu mbili za kwanza za mauzo na mahitaji bado ni makubwa mno kiasi kwamba tiketi ziliagizwa zaidi kupita kiwango cha mara 30.

Gharama ya tiketi yapaa

Makamu wa rais wa chama cha mashabiki wa soka nchini Ufaransa Mehdi Salem,amesema wanashuhudia ongezeko la gharama za tiketi kwa zaidi ya asilimia 200 tofauti na kiasi walichoambiwa na shirikisho la soka la Ufaransa na FIFA mnamo mwaka 2018.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW