1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zoezi la kuhamishwa Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina

10 Julai 2005

Jerusalem:

Naibu Waziri Mkuu wa Israeli, Ehud Olmert, amesema leo kuwa zoezi la Waisraeli kuondoka katika Ukanda wa Gaza na kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan halitachukua zaidi ya majuma mawili. Bw. Olmert amesema kuwa serikali inataka kuepusha mivutano na walowezi wa Kiyahudi na waungaji mkono wao. Kwa hiyo, imeamua kuizingira sehemu hiyo kwa miezi kadhaa kabla ya zoezi hilo kuanza Agosti 17. Naibu Waziri Mkuu wa Israeli amesema kuwa zoezi hilo ni gumu sana kwa Israeli na lenye maumivu makali. Serikali ya Israeli hapo kabla imesema kuwa operesheni ya kuwahamisha Walowezi wa Kiyahudi 8,000 katika Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huenda likachukua siyo zaidi ya mwezi mmoja.