1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zoezi la kumng'owa madarakani Donald Trump Magazetini

Oumilkheir Hamidou
18 Desemba 2019

Zoezi la kumng'owa madarakani Rais Donald Trump wa Marekani, serikali kuzidisha mapambano dhidi ya siasa kali za mrengo wa kulia na wanawake na uongozi ni miongoni mwa mada zilizogonga vichwa vya habari Ujerumani.

USA Protest in New York
Picha: picture-alliance/AP Photo/B. Matthews

Tunaanzia Marekani ambako wanachama wa Democrat wanaendelea na mchakato wa kuwahoji maafisa wa ngazi ya juu serikalini kuhusiana na tuhuma kwamba rais Trump ametumia vibaya madaraka yake. Gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linauchambua mchakato huo na kuandika: "Mtu hakosi kujiuliza kwanini mwanasiasa aliyezungukwa na magengi ya wahalifu wanaompatia ushauri na mwenye kukorofisha wazi wazi uchunguzi dhidi yake, kwanini asiwe ametimuliwa tangu zamani kutoka ikulu ya White House.

 Kumshinikiza rais wa Ukraine ampake matope mpinzani wa Trump katika uchaguzi wa rais, Joe Biden, madai ambayo ndio kitovu cha mchakato wa kumng'owa madarakani, ni sehemu moja tu ya orodha ndefu ya miko iliyovunjwa kwa aibu. Hata hivyo hakuna yeyote mjini Washington anaeamini kama kweli Trump atatimuliwa madarakani. Maoni ya wanaounga mkono ang'olewe madarakani yanatuwama kati ya asili mia 45 na asili mia 50. Idadi hiyo inatosha kumuudhi Trump na kiburi chake. Lakini kwa mapinduzi haitoshi.

Gazeti la mjini Cologne,"Kölner Stadt Anzeiger" lina maoani sawa na hayo na kuandika:"Mengi yanaonyesha mchakato wa kumpokonya madaraka utashindwa. Trump atalisherehekea hilo kwa ulimi wake mkali katika mtandao wa Twitter.

Hatua kali dhidi ya makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia

Waziri wa mambo ya ndani wa serikali kuu ya Ujerumani Horst Seehofer ametangaza azma ya serikali ya kuzidisha makali ya sheria za kupambana na makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia. Gazeti la "Badische Neueste Nachrichten" linaandika:"Mapambano ya nguvu dhidi ya hatari ya siasa kali za mrengo wa kulia yanawezekana tu ikiwa kanuni zitakuwa za aina moja kote nchini na sheria za majimbo kuhusu shughuli za polisi ambazo zinazotofautiana toka jimbo moja hadi jengine zitasawazishwa. Jamii yote inabidi iwe macho. Ubaguzi wa rangi, chuki, na mtindo ya kubaguana ni visa vinavyoshuhudiwa kila mara na katika mitandao si kazi kubwa kuifuta. Mara kwa mara inadhihirika jinsi siasa kali za mrengo wa kulia zinavyoitia sumu jamii na kuuendeya kinyume mfumo wa kidemokrasi. Kwa hivyo sote tunabidi tuwajibike."

Wanawake na uongozi

Na hatimae gazeti la "Südwest-Presse" limezungumzia mada inayohanikiza katika jamii"wanawake na uongozi". Gazeti linajiuliza:""Eti kila kitu ni bambam katika suala la usawa wa jinsia katika majukwaa ya kisiasa? Kwa bahati mbaya jibu ni "la."Na hapa suala haliwahusu wanaume wenye kiu cha madaraka na ambao wanapinga pia hilo, bali suala hapa ni pia wanawake wanaohofia viwango hivyovikiwekwa visije vikawaharibia sifa. Miaka mia moja tangu haki za wanawake zilipotangazwa, bado haki hizo hazitekelezwi kama inavyostahiki."

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW