Zoezi la kutafuta miili ya maelfu ya Wapalestina linaendelea
20 Januari 2025Msemaji wa idara ya Huduma za dharura za Kiraia ya Palestina, Mahmoud Basal, amesema wanatafuta miili ya zaidi ya watu 10,000 wanaoaminika kuwa china ya vifusi na kuongeza kuwa takriban miili 2,840 iliteketea pasi na dalili ya kupatikana kwa mabaki yake.
Usitishaji mapigano unaonekana kudumishwa
Wakaazi na madaktari huko Gaza wanasema kwa sehemu kubwa, usitishaji mapigano unaonekana kudumishwa ijapokuwa kumekuwa na matukio mengine yaliotokea.
Madaktari wanasema watu wanane wamelengwa katika mashambulizi ya Israel tangu leo asunuhi katika mji wa kusini wa Rafah bila ya kutoa maelezo zaidi.
Malori ya misaada yaanza kuingia Gaza
Nchini Israel pia hali ya mashaka inaendelea kuhusu mateka waliosalia Gaza iwapo wataweza kuokolewa katika kipindi kirefu kwa utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha vita.
Ndugu wa mmoja wa mateka waGazaAshley Waxman Bakshi, amesema wanataka kuhakikisha kuwa mwendelezo wa majadiliano ya awamu ya pili unatokea, na kuonya kuwa mambo bado.
Malori 220 ya misaada yatumwa Gaza
Takriban malori 220 ya misaada yalitumwa kutoka Misri kuelekea Ukanda wa Gaza hii leo.
Afisa wa shirika la Hilali Nyekundu wa Misri huko Sinai Kaskazini, amesema lori hizo ni pamoja na 10 za kubeba mafuta na kwamba zitaingia Gaza kupitia kivuko cha mpakani cha Keremu katika eneo la kusini.
Afisa huyo amoengeza kuwa kuna malori 3000 yaliobeba msaada wa kiutu tayari kupelekwa katika ukanda wa Gaza.
Kulingana na mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu, Tom
Fletcher, zaidi ya malori 630 yenye misaada ya kibinadamu yaliingia Gaza na angalau 300 kati yao yanapelekwa sehemu ya kaskazini ya eneo hilo la Gaza.
Vikwazo vyaondolewa dhidi ya meli zinazohusishwa na Israel
Kituo cha Kuratibu Shughuli za Kibinadamu HOOC chenye makao yake mjini Sanaa ambacho pia ni kiungo cha mawasiliano kati ya vikosi vya Kihouthi na wahudumu wa meli za kibiashara kinachohusishwa na tawi la kijeshi la Houthi, kimesema kinasitisha vikwazo dhidi ya meli zinazomilikiwa na watu binafsi au mashirika ya Marekani au Uingereza, pamoja na meli zinazosafiri chini ya bendera zao.
Usitishaji mapigano waanza kutekelezwa Gaza
Katika barua pepe iliyotumwa kwa maafisa wa sekta ya usafiri wa meli mnamo Januari 19, kituo hicho kimesema kinathibitisha kwamba katika tukio la uchokozi wowote dhidi ya Yemen kutoka kwa Marekani, Uingereza au Israeli, vikwazo hivyo vitarejeshwa dhidi ya mataifa hayo.