Zuma aendelea kugonga mwamba
19 Juni 2017Mwendesha mashitaka mkuu wa serikali Busisiwe Mkhwebane amesema leo, kwamba idara ya kupambana na rushwa nchini Afrika kusini itapinga juhudi za rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kutaka ripoti ya madai ya kuwapo ushawishi kwake binafsi na serikali yake iwekwe kando.
Thuli Madonsela, mrithi wa Mkhwebane katika wadhifa wa mwendesha mashitaka aliitoa ripoti hiyo mwezi Novemba. Ilitaka ufanyike uchunguzi wa mahakama kuhusiana na madai kuwa Zuma , baadhi ya mawaziri na baadhi ya makampuni ya taifa yalichukua hatua kinyume na utaratibu , lakini ripoti hiyo haikwenda umbali wa kueleza kwamba uhalifu ulitendeka.
Mwezi Desemba mwaka jana Zuma, ambaye amekama kutenda kosa na kukataa miito wa kutaka ajiuzulu kuhusiana na kashfa kadhaa ambazo zimeikumba serikali yake, aliitaka mahakama kuu kuweka kando ripoti hiyo.