1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uamuzi kuhusu azma ya Zuma kugombea kutolewa Afrika Kusini

9 Aprili 2024

Majaji nchini Afrika Kusini watatoa uamuzi iwapo rais wa zamani Jacob Zuma ataruhusiwa kugombea katika uchaguzi wa rais mwezi Mei.

Südafrika ehemaliger Präsident Jacob Zuma
Picha: Michele Spatarii/AP Photo/picture alliance

Zuma, ambaye anagombea kupitia chama kipya cha upinzani, amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa maafisa wa uchaguzi wa kumzuilia kushiriki uchaguzi kufuatia  kuhukumiwa mwaka 2021.

Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela mnamo Juni 2021 baada ya kukataa kutoa ushahidi mbele ya  jopo lililokuwa likichunguza madai ya ufisadi wa kifedha wakati wa uongozi wake.

ANC yashindwa katika kesi dhidi ya chama cha Zuma

Hata hivyo mawakili wake wamedai,  hukumu hiyo haina athari yoyote katika azma ya kiongozi huyo wa zamani ya kugombea kwani madai dhidi yake hayakuwa ya jinai.

Afrika Kusini itafanya uchaguzi mkuu Mei 29 katika kinyanganyiro kinachotajwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi tangu ilipoingia demokrasia nchini humo mwaka 1994.