1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zuma awataka wawekezaji wasiwe na wasi wasi

19 Septemba 2012

Afrika kusini tangu mwaka 2007 imekuwa miongoni mwa kile kinachojulikana kama washirika kumi wa kimkakati wa umoja wa Ulaya. Haya ni mataifa ambayo yanaumuhimu mkubwa kwa umoja wa Ulaya.

European Union President Belgian Herman Van Rompuy (L) and European Commission President Jose Manuel Barroso (R) welcome South African President Jacob Zuma (C) before the EU-South Africa summit at the EU headquarters in Brussels on September 18, 2012. AFP PHOTO / JOHN THYS (Photo credit should read JOHN THYS/AFP/GettyImages)
Rais Jacob Zuma (kati) akiwa na Herman van Rompuy na Jose Manuel BarrosoPicha: Getty Images

Ushirikiano huu unahusika katika nyanja za kisiasa, kiuchumi , sayansi na utamaduni. Hali hili lilionekana katika ujumbe wa Afrika kusini katika mkutano kati ya umoja wa Ulaya na nchi hiyo uliomalizika jana mjini Brussels.

Pamoja na rais Jacob Zuma , alikuwapo pia waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika kusini Maite Nkoana-Mashabane na wakuu wa idara za biasha, fedha, uchumi na teknolojia, nishati na usafiri na upande wa wenyeji alikuwapo rais wa baraza la Ulaya Herman Van Rompuy , rais wa halmashauri ya umoja wa ulaya Jose Manuel Barosso na makamishna wa masuala ya biashara , maendeleo na utafiti wa umoja huo.

Kwa upande wa biashara umoja wa Ulaya unaiweka Afrika kusini katika nafasi muhimu sana. Umoja wa Ulaya ni mshirika muhimu wa kibiashara wa Afrika kusini. Mipaka ya kibiashara haipo tena.

Tangu kutiwa saini kwa mkataba mwaka huu , zaidi ya asilimia 90 ya biashara baina ya pande hizo mbili hazijawekewa mipaka.

Ushirikiano pia na SADC

Umoja wa Ulaya unapendelea kupiga hatua moja zaidi na kufikiwa kwa makubaliano ya ushirikiano pamoja na jamii yote ya mataifa yaliyo wanachama katika jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika , SADC.

Katika jumuiya ya SADC yanakutikana mataifa yote yaliyoko kusini mwa bara hilo, Afrika ya kusini binafsi ikiwa inachukua nafasi ya mbele ya uongozi. Hadi sasa lakini Afrika kusini inakuwa ndio inatia guu katika kupatikana makubaliano kama hayo, huenda ni kwasababu Afrika kusini inafaidika kwa sasa na makubaliano hama hayo na umoja wa Ulaya.

Rais Jacob Zuma amekiri katika mkutano na waandishi habari mjini Brussels , kuwa katika suala hili hatujapiga hatua kubwa , matokeo muhimu bado yanategemea masuala ya dharura, katika kuonesha maelewano na hali inayobadilikabadika.

Ni katika nyanja gani basi umoja wa Ulaya unapaswa kutoa hali ya uelewa zaidi pamoja na hali ya kubadilika, hilo hakuliweka wazi rais Zuma.

Kwa upande mwingine ameonyesha hali ya kuondoa uwezekano wa matarajio. Tangu Januari mosi mashirika ya ndege , viwanja vya ndege vya Ulaya kulipia kodi ya gesi zinazoharibu mazingira. Na makubaliano haya yanayakumba pia mashirika ambayo si kutoka bara la Ulaya.

Sio tu Marekani na China ambazo zinadai kuwa hali hiyo ni kinyume na sheria kwa mashirika ya ndege na abiria, lakini hata nchini Afrika kusini, ambapo rais Zuma binafsi analitambua hilo.

"Wakati tunaheshimu haki ya umoja wa Ulaya katika eneo lake, tunatambua pia matokeo ambayo hayakutarajiwa kuhusu uhusiano na wanachama wengine wa jamii ya kimataifa".

Kiwingu kimetanda

Kiwingu kimetanda tangu kuanza kwa majira ya joto mwaka huu kuhusiana na uhusiano kati ya Afrika kusini na umoja wa Ulaya. Mwezi August polisi wa Afrika kusini waliwapiga risasi wafanyakazi wa mgodi wa Platinum wa Marikana 34.

Wafanyakazi wa mgodi wa Marikana wakiwa wamegomaPicha: picture-alliance/dpa

Picha zilionekana duniani kote , ambazo zinakumbusha wakati wa utawala wa kibaguzi, lakini tu wakati huu ni Waafrika wakipambana na Waafrika wenzao. Katika tukio hilo Afrika kusini haiangiliwi tu katika upande wa kiutu. Nchi hiyo pia iliingiwa na wasi wasi kuhusu uwekezaji kutoka nje.Mgodi huo wa Marikana unamilikiwa na kampuni kutoka Uingereza. Van Rompuy , anaiweka hali hiyo katika suala la matatizo ya kijamii nchini Afrika kusini , ambapo alilijadili pamoja na rais Zuma.

Rais wa baraza la Ulaya Herman van RompuyPicha: ap

"Tatizo hili limekuwa kubwa zaidi katika muktadha wa ghasia za migodini zilizotokea nchini Afrika kusini. Tukio lililotokea katika mgodi wa Marikana lilikuwa ni maafa na tunaunga mkono tume ya uchunguzi iliyoundwa na rais Zuma".

Rais Jacob Zuma amesisitiza jana kuwa wawekezaji wa kimataifa wasiwe na wasi wasi kuwekeza nchini Afrika kusini. Wakati huo huo vyombo vya habari nchini Afrika kusini vimesifu kumalizika kwa migomo migodini nchini humo baada ya wafanyakazi kukubali pendekezo la wamiliki wa mgodi wa madini ya Platinum , Lonmin kuongeza mshahara kwa asilimia 22. Lakini vyombo hivyo vya habari vimetahadharisha kuwa ongezeko hilo linaweka mtazamo wa hatari katika sekta hiyo.

Mwandishi : Christoph Hasselbach / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Yusuf Saumu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW