1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZURICH. Nchi za umoja wa Ulaya zaanza sheria ya kuyapiga marufuku baadhi ya mashirika ya ndege

2 Septemba 2005

Uswisi imetoa orodha yake ya mashirika ya ndege ambayo yamepigwa marufuku kutua nchini humo.

Hatua hiyo inafuatia baada ya Ufaransa na Ubelgiji kutangaza orodha zao wiki moja iliyopita.

Orodha iliyotolewa na wizara ya uchukuzi ya Uswisi imetaja mashirika ya ndege ya Flash ya Egypt na Shirika la ndege la Armenia kwamba hayataruhusiwa kutua katika viwanja vyake vya ndege.

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ilipitisha azimio mwezi februari, kwamba nchi za umoja wa ulaya ziwe na msimamo mmoja kuhusu mashirika ya ndege yaliyo pigwa marufuku na nchi zingine wanachama wa umoja azimio ambalo kwa sasa limeanza kutumika rasmi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW